Audio

Mazingira Mtaani (Environment in the Hood) (Introduction to a radio program about human wildlife conflict. In Swahili.) mp3 5.97 MB
Mazingira Mtaani (Environment in the Hood) (Feature interviews from the radio show about human wildlife conflict. In Swahili.) mp3 7.71 MB

© Mary Mwenda, 2011. All Rights Reserved.

1 response to Audio

  1. And here is the script for program 1:

    MAZ MTAANI PGM 1
    It is my pleasure to welcome you my listener to this new Mazingira mtaani ( Environment in the hood ) program.This is a very new program that highlights issues affecting our environment.Some of the issues we shall be handling are, climate change,how it affects you and how to mitigate and adopt to it.This program will also be giving you a chance to participate by calling or sending us a text here in the studio about the program.This will be a forum where you will let us know what is happening to your environment and how you are affected.This program comes you way every wedsday from 4.15 -4.30 pm here at Pamoja fm 99.9.welcome to the program.
    Am your presenter …Mary mwendwa.

    Hujambo msikilizaji wangu, ni furaha yangu tena kwa kuungana nawe katika kipindi hiki kipya kabisa, kipindi kinachojulikana kama mazangira mtaani, kipindi cha kukuelimisha mengi kuhusu mazingira yako, kipindi cha kukujuza mengi kuhusu matukio mengi kuhusu hali ya mabadiliko ya hali ya anga (climate change) na vile unavyopaswa kupambana na hali hii , kipindi hiki pia kitakupa nafasi wewe kama msikilizaji kuchangia kupitia kwa simu yale ambayo yanatendeka katika maoeneo unayoishi na vipi yanaathiri mazingira yako.kumbuka kipindi hiki kitakuwa kinakujia kila jumatano kwanzia saa kumi na nusu jioni hadi saa kumi na dakika arubaini na tano hapa pamoja fm 99.9.Karibu kwenye kipindi…jina langu ni …Mary Mwendwa
    Bridge: play up then under 0.08 sec
    Naam, bila shaka vile umesikia hiki ni kipindi kuhusu mazingira mtaani, kipindi cha robo saa kinachokufikia hapo ulipo kwanzia saa kumi na nusu hadi saa kumi na dakika arubaini na tano za jioni hapa pamoja fm 99.9 .Vile nimekuelezea hapo awali mzikilizaji wangu, kipindi hiki kitakujuza mengi kuhusu mazingira yako, baadhi ya yale tutakuwa tukiyaangazia ni kama vile mabadiliko ya hali ya anga na mengi neyo hukusu mazingira .Kupitia kwa mfululizo wa vipindi hivi nina imani kuwa utakuwa mmoja wa wale ambao watajumuika na wengine katika utunzaji wa mazingira.Hivi maajuzi tumempoteza mwendazake Mama Wangari Maathai ambaye amechangia pakubwa sana kwa utunzaji wa mazingira kupitia kwa harakati zake za upandaji wa miti hapa nchini.Kwa kweli tutamkumbuka na mungu ailaze roho yake mahali pema .Katika kipindi cha leo tutakuwa tukiangazia swala kuu ambalo kwa wengi wetu huwa tunalishuhudia mara kwa mara kibinafsi au kupitia kw a vyombo vya habari.Nalo ni Uhasama baina ya wanyama wa pori na binadamu.Kwa kweli nafahamu ni vigumu sana, tusema simba amewavamia mifugo wako na kuwala, ni jambo la kukera sana , na mara mingi huwa tunaelekeza kidole cha lawama kwa shirika la kutunza wanyama wa pori.Lakini, umewahi kufikiria kuwa, unapotoa uhai wa wanyama wa pori unachangia pakubwa kwa kutotunza mazingira?na pia kumbuka uchumi wa nchi hii unategemea wanyama wa pori kwa kiwango Fulani kupitia kwa wataalii ambao hutembelea mbuga za wanyama?Leo katika sehemu yetu ya Makala,nilitembelea shirika la Bornfree , ambalo linishigulika na kuhamasisha watu kuhusu kulinda wanyama wa pori, tutakuwa tukizungumza naye msimamizi wa shiriki hili hapa nchini Kenya,Bw.Iregi Mwenja, lakini kabla ya hayo, nitapunga hewa kidogo na uweze kuburudika kwa wimbo utwatao.
    Song : 4 min
    Kipindi ni mazingira mtaani , na kumbuka leo tunaangazia uhasama baina ya binadamu na wanyama wa pori.Katika sehemu ya makala yetu leo, Bw.Iregi Mwenja kutoka shirika la Bornfree atakuwa akitueleza mengi na harakati zao kama shirika la Bornfree kuhusu swala hili.Basi bila kupoteza muda tutajiunga naye Bw.Iregi .
    Makala: Bornfree
    Bridge
    Nina imani kuwa umeelimika kuhusu uhasama baina ya binadamu na wanyama wa pori, ( human wildlife conflict )Jambo ambalo limejitokeza wazi ni kwamba, ni jukumu langu mimi na wewe kuweza kuhakikisha kuwa wanyama wa porini wapo salama.endapo una swali au pendekezo lolote kuhusu kipindi hiki …usisite kuwasiliana nasi kupitia nambari hizi
    0751 02 13 25
    0751 02 13 25
    Bridge
    Sasa nitamkaribisha mwenzangu jirongo luyali katika sehemu yetu ya yaliyojiri katika mazingira.Karibu.
    Bridge
    Yaliyojiri katika mazingira
    Bridge
    Na kufikia hapo ndipo tunafika mwisho wa kipindi hiki kwa leo, kumbuka kuungana name juma lijalo wakati kama huu , yani saa kumi na nusu hadi saa kumi na dakika kumu na tano jumatano jioni.Sina linguine bali nakuomba utunze mazingira yako.Kutoka hap amzangira mtaani ni mimi wako.
    Mary mwendwa.

Leave a reply

You must be logged in to post a comment.